EAD ni nini | Hati ya Idhini ya Ajira| USAHello (2024)

Ukurasa huu umetafsiriwa pia katika:

  • English (Kiingereza),
  • العربية (Kiarabu),
  • 简体中文 (Kichina),
  • فارسی/دری (Kiajemi),
  • Français (Kifaransa),
  • Kreyòl Ayisyen (Mhaiti),
  • پښتو (Kipashto),
  • Русский (Kirusi),
  • Español (Kihispania),
  • українська (Kiukreni),
  • Tiếng Việt (Kivietinamu)

Wahamiaji wengi huja USA kufanya kazi. Ikiwa wewe si raia wa Marekani au mmiliki wa Green Card, ni lazima uwe na Hati ya Idhini ya Ajira (EAD). Pata taarifa kuhusu namna ya kuomba kibali cha kufanya kazi na kukifufua.

Imesasishwa Aprili 8, 2024

Je, EAD ni nini?

EAD ni Hati ya Idhini ya Ajira au kibali cha kufanya kazi. Ili kufanya kazi nchini Marekani, ni lazima uwe raia wa Marekani, mkazi halali wa kudumu, au uwe na kibali cha kufanya kazi. EAD inathibitisha kuwa unaweza kufanya kazi kihalali nchini Marekani.

Waajiri lazima wakague kama umeidhinishwa kufanya kazi ili kufuata sheria na kuepuka faini. Ni kawaida kwa waajiri kuuliza wakati wa mahojiano ya kazi, “Je, umeidhinishwa kisheria kufanya kazi nchini Marekani?”

EAD si mahsusi kwa mwajiri husika. Unaweza kutumia kadi ya EAD kufanya kazi kwa mwajiri yeyote nchini Marekani.

Kadi ya EAD

Kadi ya EAD inajumuisha jina lako, picha, nambari ya mgeni, nambari ya kadi, tarehe ya kuzaliwa, alama za vidole na tarehe ya mwisho wa matumizi. Unaweza kutumia kadi hii kama kitambulisho. Si hati halali ya kuingia tena Marekani. Kadi hii pia inajulikana kama I-766.

EAD ni nini | Hati ya Idhini ya Ajira| USAHello (1)
EAD ni nini | Hati ya Idhini ya Ajira| USAHello (2)

Je, nani anaweza kupata EAD?

Utahitaji kuwa katika kategoria yenye ustahiki ili kuomba EAD.

Baadhi ya kategoria hizi ni:

  • Mkimbizi
  • Mtafuta Hifadhi
  • Msamahewa wa kibinadamu
  • Hali ya Kulindwa kwa Muda (TPS)
  • Hairisho la Kuondoka Kwa Shurti (DED)
  • DACA
  • VAWA
  • Viza ya U na T
  • Msubiri Hifadhi (siku 150 baada ya kuwasilisha maombi)
  • Zuio la kuf*ckuzwa au kuondolewa
  • Baadhi ya watu wasio wahamiaji wanaotegemea ajira
  • Wanandoa, wachumba au wategemezi wa kategoria fulani zilizoidhinishwa

Pata orodha kamili ya kategoria zinazostahiki.

Raia wa Marekani na wamiliki wa Green Card hawahitaji EAD kufanya kazi.

Watafuta hifadhi

Ikiwa wewe ni mtafuta hifadhi mwenye maombi yanayosubiri, ni lazima usubiri siku 150 kabla ya kuomba EAD. USCIS inaweza kukataa Fomu yako ya I-765 ikiwa utaiwasilisha kabla ya muda wa kusubiri wa siku 150.

Mradi wa Utetezi wa Watafuta Hifadhi (ASAP) ni rasilimali muhimu.

(https://www.youtube.com/watch?v=BZ2SOUPbcZY)

Wakimbizi na wahamiaji

Wakimbizi na wahamiaji wameidhinishwa kiotomatiki kufanya kazi nchini Marekani. Huna haja ya kutuma maombi au kulipa ada ya EAD.

Ikiwa wewe ni mkimbizi, USCIS itashughulikia kiotomatiki Fomu yako ya I-765 mara tu utakapowasili Marekani. Mara tu ombi lako litakapoidhinishwa, watakutengenezea EAD yako. Utapata kadi yako ya EAD kwa njia ya posta ndani ya siku 30. Unaweza kutumia Fomu yako ya I-94 kama uthibitisho kwamba unaweza kufanya kazi wakati ukisubiri kadi yako.

Ikiwa wewe ni mtafuta hifadhi, huhitaji kuomba idhini ya kazi. Unapopewa hifadhi, unaidhinishwa mara moja kufanya kazi.

Wasamehewa wa Afghanistan na Ukraine

Baadhi ya wasamehewa wa Afghanistan na Ukraine hawahitaji kusubiri idhini ya Fomu I-765 ili kufanya kazi Marekani. Fomu yako ya I-94 ambayo muda wake haujaisha inaweza kuwa uthibitisho kwamba unaweza kufanya kazi kwa siku 90 za kwanza kazini mwako. Baada ya hapo, utahitaji kuonesha EAD na kadi ya ‘Social Security’ isiyo na vizuizi.

USCIS pia inatoa misamaha ya ada na ushughulikiaji wa haraka zaidi. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye kurasa zao za Afghan Nationals na Uniting for Ukraine.

Jinsi ya kuomba EAD

Ikiwa wewe si mkimbizi au mtafuta hifadhi, utahitaji kuomba kibali cha kufanya kazi kupitia USCIS.

Hii ni orodha ya hatua za kufuata:

1. Soma maelekezo. Fomu hii inachanganya. Inashauriwa kupata usaidizi wa kisheria ili kuepuka makosa.

2. Kusanya nyaraka zinazohitajika. Utahitaji nakala ya kitambulisho kilichotolewa na serikali na picha za ukubwa wa pasipoti. Zipo hati zingine zinazohitajika kulingana na kategoria yako.

3. Jaza na usaini Fomu I-765. Unaweza kufanya hivi mtandaoni au kwa kuichapa fomu. Hakikisha unajibu maswali yote. Ukiichapa fomu, hakikisha unaisaini kwa mkono.

4. Lipa ada ya kuwasilisha maombi. Unapaswa kulipa $470 kwa maombi ya mtandaoni au $530 kwa maombi ya karatasi. Ambatisha risiti yako ya ada ya kuwasilisha maombi kwenye ombi lako la EAD. Huenda usilazimike kulipa ada ikiwa una hali fulani ya uhamiaji au una msamaha wa ada ulioidhinishwa.

5. Toa nakala ya fomu. Hii ni muhimu ikiwa unahitaji kufufua EAD yako au ikipotea au kuibiwa.

6. Wasilisha fomu yako. Una chaguo la kuwasilisha kwa barua pepe au mtandaoni. Ikiwa unawasilisha kwa barua na unataka kupokea arifa za kielektroniki, jumuisha Fomu G-114.

7. Tunza nambari yako ya risiti ya USCIS. Hivi ndivyo unaweza kufuatilia maombi yako.

8. Lazima usubiri idhini kabla ya kuanza kufanya kazi. Unaweza kuanza kutafuta kazi huku ukisubiri.

Iwapo utaarifiwa kwamba unahitaji huduma za bayometriki, utapokea notisi ya miadi iliyo na maelekezo. Hii itagharimu $85 ya ziada. Watafuta hifadhi wenye maombi yanayosubiri hawahitaji kulipa ada hii. Kulipa kiasi kisicho sahihi inaweza kusababisha maombi yako kukataliwa.

Ikiwa unajaza kupitia fomu nyingine, lazima ufuate maelekezo ya fomu nyingine. Kwa mfano, ikiwa unajaza Fomu I-765 kupitia Fomu I-539, lazima uwasilishe fomu zote mbili ambapo Fomu I-539 inakuelekeza. Pia, angalia ikiwa ada za fomu tofauti lazima zilipwe mbali mbali. Vinginevyo, fomu yako inaweza kukataliwa.

Muda wa kusubiri EAD

Muda wa kusubiri unaweza kutofautiana kulingana na hali ya uhamiaji na kituo cha huduma. Unaweza kuangalia muda wa jumla wa ushughulikiaji wa maombi mtandaoni. Unaweza pia kuona makadirio ya muda wa kusubiri maombi yako kwa kuingia katika akaunti yako ya myUSCIS. Baada ya USCIS kupokea maombi yako, watakutumia pia nambari ya risiti ili kufuatilia hali ya maombi yako.

Ikiwa wewe ni mkimbizi, utapata EAD yako ndani ya siku 30 baada ya kuwasili Marekani.

Ikiwa una ombi la hifadhi linalosubiri, muda wa kushughulikia maombi ni siku 30. Hii ni nyongeza ya siku 150 ambazo lazima usubiri kabla ya kutuma maombi. Muda ambao maombi ya hifadhi yanasubiri kabla ya kupata EAD hujulikana kama “muda wa siku 180 wa EAD ya watafuta hifadhi.”

Ikiwa wewe ni mhudumu wa afya au mfanyakazi wa huduma za watoto, unaweza kupata mchakato wa haraka au wa kasi ikiwa una mojawapo ya yafuatayo:

  • Fomu ya awali ya EAD ambayo imekuwa ikisubiri kwa zaidi ya siku 90
  • Fomu inayosubiri ya kufufua EAD na EAD iliyokwisha muda wake au inayoisha muda ndani ya siku 30 au chini ya hapo.

Mwisho wa matumizi ya EAD

Kwa sasa EAD inaweza kutumika kwa hadi miaka 5 kulingana na hali yako ya uhamiaji. Sheria mpya inasema EAD yako itakuwa halali kwa miaka 5 ikiwa:

  • Umekubaliwa au kusamehewa kama mkimbizi
  • Umepewa hifadhi
  • Umepewa zuio la kuf*ckuzwa au kuondolewa, urekebishaji wa hali, au sitisho la kuondolewa
  • Una maombi yanayosubiri ya hifadhi au zuio la kuondolewa, sitisho la kuondolewa, au urekebishaji wa hali

Kanuni hii inatumika tu kwa maombi yaliyowasilishwa mnamo au baada ya Septemba 27, 2023. Haitumiki kwa EAD zilizotolewa kabla ya tarehe hii. Hali nyingine za uhamiaji, kama vile TPS, zinaweza kuwa na EAD ambazo ni halali kwa viwango tofauti vya muda. USCIS pia inaweza kuendeleza kiotomatiki EAD kwa nchi zenye TPS.

Kufufua EAD

Ikiwa EAD yako inakwisha hivi karibuni au imeisha muda wake, unaweza kuomba kuifufua. Lazima uwasilishe Fomu mpya ya I-765. Utahitaji kulipa tena ada ya maombi isipokuwa kama umekidhi misamaha fulani au uwe na msamaha wa ada ulioidhinishwa.

Unaweza kuwasilisha ombi lako la kufufua siku 180 kabla ya tarehe ya mwisho wa matumizi. Ni bora kutuma maombi mapema ili usiwe na pengo katika idhini ya ajira.

Kwa wale walio katika kategoria yenye ustahiki, EAD yako itaendelezwa kiotomatiki kwa siku 540 ikiwa:

  • Uliwasilisha maombi ya kufufua EAD yako mnamo au baada ya Oktoba 27, 2023 na ilikuwa bado haijashughulikiwa mnamo Aprili 8, 2024.
  • Uliwasilisha maombi ya kufufua EAD yako kati ya Aprili 8, 2024 na Septemba 30, 2025

Wanaostahiki uendelezaji wa kiotomatiki ni wakimbizi, watafuta hifadhi, watafuta hifadhi wanaosubiri, wenye TPS, waombaji wa awali wa TPS wanaosubiri, waombaji wa VAWA, na wengine. Tazama orodha kamili ya kategoria zinazostahiki na maelezo zaidi.

Kikokotoo cha Uendelezaji wa EAD cha USCIS kinaweza kukusaidia kubaini tarehe sahihi ya mwisho wa matumizi.

Nambari ya ‘social security’

Ili kufanya kazi nchini Marekani, utahitaji pia kuwa na ‘Social Security Number’ (SSN). Unaweza kuomba SSN na kadi yako ya EAD kwa wakati mmoja kupitia Fomu I-765. Nambari ya ‘Social Security’ inatumiwa kuripoti mshahara wako kwa serikali na kufanya ubainifu wa mafao.

Tafuta usaidizi

Ni muhimu kutafuta ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria wa uhamiaji au mwakilishi aliyeidhinishwa ikiwa una maswali au wasiwasi wowote. Mashirika na wanasheria wengi hutoa huduma za kisheria bila malipo au kwa gharama nafuu.

Msaada kuhusiana na kulipa ada

Unaweza kuomba msamaha wa ada ikiwa kaya na kipato chako vina ukubwa fulani. Ni lazima uwasilishe Fomu I-912 pamoja na ombi lako la EAD au uwasilishe barua ya kuomba msamaha wa ada pamoja na ushahidi unaohitajika.

Kadi ya EAD iliyopotea au kuibiwa

Unaweza kupata EAD mbadala ikiwa kadi yako imeibiwa, imepotea au imeharibika. Utahitaji kuwasilisha Fomu mpya ya I-765 ili kubadilishiwa EAD.

Kufanya kazi bila idhini

Watu wengi hawana hadhi ya kisheria ya uhamiaji nchini Marekani na hivyo hawawezi kupata EAD. Mara nyingi hufanya kazi za “vibarua” au hulipwa kwa pesa taslimu. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu wafanyakazi wasio na vibali.

Kuwa na kazi au kutoa huduma bila hati sahihi ni kinyume cha sheria za kazi na uhamiaji za Marekani. Kufanya kazi kwa muda, kufanya kazi mtandaoni, au kuendesha biashara yako bila idhini kunaweza kuwa na madhara makubwa. Viza yako inaweza kusitishwa au unaweza kuf*ckuzwa nchini.

Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa USCIS na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

More from USAHello

Looking for specific information?

Tafuta usaidizi wa kisheria

Using USCIS tools

Biometrics appointment

Paying USCIS fees

Immigration status and benefits for Afghans

Ukrainian parolee benefits

EAD ni nini | Hati ya Idhini ya Ajira| USAHello (2024)

References

Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Tish Haag

Last Updated:

Views: 6070

Rating: 4.7 / 5 (67 voted)

Reviews: 90% of readers found this page helpful

Author information

Name: Tish Haag

Birthday: 1999-11-18

Address: 30256 Tara Expressway, Kutchburgh, VT 92892-0078

Phone: +4215847628708

Job: Internal Consulting Engineer

Hobby: Roller skating, Roller skating, Kayaking, Flying, Graffiti, Ghost hunting, scrapbook

Introduction: My name is Tish Haag, I am a excited, delightful, curious, beautiful, agreeable, enchanting, fancy person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.